Hofu ya kutokea vurugu baada ya uchaguzi mkuu Oktoba 25 imezidi kutanda mkoani Mtwara ambapo sasa idadi ya wananchi husasan watoto na wanawake wanaohama mkoa huo inazidi kuongezeka.

Kwa mujibu wa taarifa iliyoripotiwa na Idhaa ya Kiswahili ya ‘DW’, hofu zaidi imezidi kutanda hasa kutokana na kuonekana kwa baadhi ya vifaa vya jeshi na wanajeshi wakiwa kwenye vifaru wakiingia katika mkoa huo.

Wananchi wengi wanayakumbuka machafuko yaliyotokana na mzozo wa gesi asilia mkoani humo mwaka 2013, hivyo hiyo inatajwa kuwa kati ya sababu ya hofu hiyo.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi limetangaza kuwa litaimarisha ulinzi mkali katika maeneo yote nchini ili kuhakikisha kuwa kila raia mwenye sifa za kupiga kura anapiga kura kwa amani na utulivu. Pia, Jeshi hilo lilitoa onyo kwa wote wanaopanga kufanya vurugu ya aina yoyote kuacha mara moja kwani watachukuliwa hatua kali.

 

 

Lazar Markovic Afungaka Kuhusu Brendan Rodgers
Pellegrini: De Bruyne Ametupa Heshima