Bara la Afrika, limekuwa ni nyumbani kwa baadhi ya watu ambao ni matajiri zaidi duniani ambapo hivi majuzi jarida la Forbes Africa, lilitoa orodha yake ya watu matajiri zaidi barani 2023, ikiwa na mchanganyiko wa majina yanayofahamika na yale ya wageni.
Orodha hiyo, inajumuisha watu binafsi kutoka sekta mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mawasiliano ya simu, benki, madini, na taasisi nyinginezo, huku orodha ya mwaka huu ikiwa na mabadiliko kadhaa kutokana na hali ya kiuchumi ya bara hili ambayo imeendelea kubadilika.
Mwanzilishi na Rais wa Dangote Group, Aliko Dangote ndiye mtu tajiri zaidi barani Afrika, akiwa na utajiri wa dola bilioni 13.5 huku utajiri wake ukitokana na kampuni yake ya kutengeneza saruji (Dangote Cement), ambayo inafanya kazi katika nchi kadhaa za Afrika, zikiwemo Nigeria, Zambia, Afrika Kusini na Tanzania.
Kupitia orodha ya kila mwaka ya watu matajiri zaidi barani Afrika kwa 2023, ambayo inajumuisha mabilionea 19 kutoka nchi saba, inaonesha kuwa mabilionea hao 19 wa bara hili, wana thamani ya takriban dola bilioni 81.8, pungufu toka dola bilioni 84.9 iliyokuwa ikishikiliwa na mabilionea 18 wa bara hilo mwaka mmoja uliopita (2022).
Hata hivyo, anguko hilo la kiwango cha pamoja cha utajiri linatokana kushuka kwa soko la kimataifa la mwaka 2022, kulikosababishwa na janga la Uviko-19 na sababu zingine ikiwemo vita vya Urusi na Ukraine, huku Dangote akisalia kileleni mwa orodha hiyo kwa mwaka wa 12 mfululizo.
Anayeshika nafasi ya pili ni Johann Rupert, yeye ni Mwenyekiti wa kikundi cha bidhaa za anasa cha Richemont akiwa utajiri wa dola 10.7 bilioni akifuatiwa na Nicky Oppenheimer mwenyekiti wa zamani wa De Beers, na utajiri wake ni dola bilioni 8.4 wote wakiwa wanatoka nchini Afrika Kusini.
Nassef Sawiris wa Misri, ambaye ana hisa katika Adidas na anaendesha OCI, mojawapo ya wazalishaji wakubwa wa mbolea ya nitrojeni duniani, anachukua nafasi ya tano akiwa na utajiri wa dola bilioni 7.2, huku Mike Adenuga, mmiliki wa kampuni kubwa ya mawasiliano ya Globacom na kampuni ya mafuta ya Conoil Producing, akishika nafasi ya sita.
Nchini Tanzania tunaye Mohammed Dewji, ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Mohamed Enteprises akiwa na utajiri wa dola bilioni 1.3 akifuatiwa na Othman Benjelloun wa Morroco mwenye utajiri wa dola 1.2 bilioni na wa 19 ni Folorunsho Alakija wa Nigeria mwenye utajiri wa dola milioni 800.
Hii hapa ni orodha kamili:
1. Aliko Dangote (Nigeria) – $13.5 billion
2. Johann Rupert (South Africa) – $10.7 billion
3. Nicky Oppenheimer (South Africa) – $8.4 billion
4. Abdulsamad Rabiu (Nigeria) – $7.6 billion
5. Nassef Sawiris (Egypt) – $7.2 billion
6. Mike Adenuga (Nigeria) – $5.6 billion
7. Issad Rebrab (Algeria) – $4.6 billion
8. Naguib Sawiris (Egypt) – $3.3 billion
9. Mohamed Mansour (Egypt) – $3 billion
10. Patrice Motsepe (South Africa) – $2 billion
11. Isabel dos Santos (Angola) – $1.8 billion
12. Strive Masiyiwa (Zimbabwe) – $1.7 billion
13. Koos Bekker (South Africa) – $1.5billion
14. Aziz Akhannouch (Morocco) – $1.4billion
15. Mohammed Dewji (Tanzania) – $1.3billion
16. Othman Benjelloun (Morocco) – $1.2billion
17. Youssef Mansour (Egypt) – $900 million
18. Yasseen Mansour (Egypt) – $800 million
19. Folorunsho Alakija (Nigeria) – $600 million