Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amesema Jeshi la Polisi limejiimarisha katika upande wa mafunzo mbalimbali ya medani kwa ajili ya kukabiliana na matishio ya uhalifu na wahalifu pamoja na kuhakikisha hali ya usalama nchini inaendelea vizuri.
IGP Sirro amesema hayo leo jijini Tanga wakati alipofanya ziara ya ukaguzi katika eneo la kambi ya mafunzo ya medani za kivita ambapo zaidi ya askari 700 wa cheo cha Mkaguzi wa Polisi wanapatiwa mafunzo ya medani katika eneo hilo.
Afikishwa Mahakamani kwa kubaka mtoto
Aidha, Sirro amesema katika kuelekea miaka 60 ya Uhuru, Jeshi la Polisi limejipanga katika kuhakikisha amani na utulivu vinaimarika nchini. Pia amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi hilo ili kufichua uhalifu na wale watakaojaribu kuvuruga amani ya nchi watashughulikiwa kwa mijibu wa sharia.
Kwa upande wake Kamishna wa Operesheni na Mafunzo CP Liberatus Sabas, amesema kuwa Jeshi la Polisi limefanikiwa kukamilisha ujenzi wa kambi za midani za kivita lililopo Mkomazi mkoani humo.