Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Kristalina Georgieva amezitaka Serikali za Mataifa Duniani kote kutoa ruzuku kwa ajili ya gharama za chakula na nishati kwa wananchi wasiojiweza hasa masikini.
Hatua ya inatokana na watu wengi ulimwenguni kote kukabiliwa na upandaji wa gharama za maisha ambapo amedai watu hao wanahitaji msaada wa hali na mali ili kuwakomboa.
“itafutwe namna ya usaidizi na hasa ikiwezekana iwe kwa kutoa ruzuku moja kwa moja kwa watu sababu Serikali nyingi zinatoa msaada lakini wakosoaji wanahoji kuwa hiyo haitoshi,” ameongeza Georgieva.
Amesema Linapokuja suala la gharama ya maisha magumu vipo vipaumbele viwili ambavyo ni kuwatizama watu maskini na.makundi makundi ya jamii ambayo kwasasa yanakabiliwa na upandaji wa bei za vyakula na nishati.
Majukumu ya IMF ni kufanya kazi na serikali za mataifa mbalimbali ili kuleta utulivu wa uchumi wa Dunia na kuimarisha ustawi wa jamii jambo ambalo linakabiliwa na changamoto hasa rekodi za mwaka 2022 za kupanda kwa bei ya vyakula, mafuta na gesi.
Hatua hii imefanya kundi la mashirika ya maendeleo ya kimataifa, IMF na Benki ya Dunia kuzindua mpango mkubwa wa kujaribu kukabiliana na uhaba wa chakula duniani kote mapema wiki hii.