Rais Mstaafu Jakaya Kikwete amepewa tuzo ya heshima iliyotolewa na Taasisi ya United cities and Local government of Africa (UCLG Africa), iliyopokelewa kwa niaba yake na Waziri wa Ardhi Nyumba na maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula.

Waziri Mabula amepokea tuzo hiyo ya (Commitment in Fevour of the African Movement of the Territorial Government), katika mkutano wa Viongozi wa Mataifa, viongozi wa miji, wataalam na wadau uliokuwa ukijadili maendeleo ya miji barani Afrika ambao umemalizika hii leo Mei 22, 2022 Kisumu nchini Kenya.

Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa kwenye mkutano huo wa kimataifa maarufu kwa jina la “Africities” ni hali ya miundo mbinu kwenye miji na namna bora ya kuimarisha maisha ya wakazi wa maeneo husika.

“lengo ilikuwa ni kutafuta suluhu ya changamoto zinazowasumbua wakazi wa miji yao kama vile mipangilio mibaya ya majengo, mitaa pamoja na changamoto za  upatikanaji wa umeme,” ameeleza mtaalam makazi kutoka jiji la Nairobi Celestin Baraza

Kauli mbiu katika mkutano huu ilikuwa ni “mchango wa miji inavyoweza kuchangia utekelezwaji wa dira ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2030 na Umoja wa Afrika mwaka 2063”.

Majiji mengine ambao yamewahi kuandaa mkutano huu unaofanyika kila baada ya miaka mitatu tangu1998 ni Abidjan nchini Ivory Coast, Johannersburg – Afrika ya Kusini, Dakar – Senegal na Marakesh – Morocco.

IMF yatoa ruzuku kwa wananchi
Ngono ya mdomo inavyoeneza maambukizi ya Ukimwi