Usafiri wa reli nchini India ni muhimu sana ambapo kwa siku, abiria zaidi ya milioni 20 hutumia usafiri huo, leo Serikali imetangaza kufungua tena huduma ya usafiri wa reli na itaendesha treni chache.
Treni maalumu zitaanza kufanya tena kazi katika majiji makubwa ikiwemo New Delhi na Mumbai, wakati nchi hiyo ikianza kulegeza vizuizi vyake vya karibu wiki saba, wakati maambukizi ya virusi vya corona yakiongezeka.
Abiria wataruhusiwa kuingia kwenye vituo vya treni baada ya kupimwa joto la mwili, kuheshimu umbali kati ya mtu na mtu na kupewa dawa za kujitakasa mikono.
Usafiri wa reli, barabara na anga ulisitishwa mwishoni mwa mwezi Machi kama sehemu ya hatua kali za nchi nzima za kukabiliana na covid-19.