Iran imeyakana madai ya Israel kuhusu kuwepo kwa nyaraka za siri kutoka Tehran zinazothibitisha kuwa bado inaendelea na mpango wake wa Nyuklia.
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amesema kuwa kuna nyaraka ambazo zinaonyesha kuwa Iran inaendelea na mpango wake wa Nyuklia hata baada ya kusaini mkataba wa mwaka 2015 wa kuachana na mpango huo.
Aidha, Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu ameituhumu Iran kuwa inaendelea na mpango wake wa Nyuklia mbali na kusaini makubaliano ya Umoja wa Mataifa wa kuachana na mpango huo.
”Iran imefanya ulaghai kuhusu kuachana na silaha za nyuklia, nyaraka zaidi ya mia moja zinaonyesha hivyo, pili hata baada ya makubaliano ya kuacha, Iran imeendelea kutunza na kukuza mpango wake wa nyuklia kwa matumizi ya baadaye, tatu Iran imedanganya tena mwaka 2015 na mwisho makubaliano yote yamejaa uongo mtupu,”amesema Netanyahu
Kwa upande wake kiongozi wa kidini wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei amekanusha madai hayo na kusema kuwa nchi yake itajibu kama Marekani itafanya maamuzi yoyote ya kuwaumiza.
Hata hivyo, Rais wa Marekani, Donald Trump amesema kuwa Netanyahu ametoa taarifa muhimu kuhusu suala la Iran kuendela na mpango wa nyuklia ambao haukabaliki.
-
UN kuupigia kura mgogoro wa Sahara Magharibi
-
Korea Kaskazini yakubali kusitisha mpango wake wa nyuklia
-
Trump atishia kuifunga tena Serikali kuu ya Marekani