Waziri Mkuu wa Israeli, Benjamin Netanyahu amesema kuwa Iran inawapa Syria silaha zenye ubora zaidi ambazo ni tishio kwa Israel hivyo ni vyema kuikabili mapema kuliko kusubiri baadae.
Ameyasema hayo wakati akihutubia bunge la nchi hiyo, ambapo amesema kuwa wamedhamiria kuikabili Irani dhidi ya uchokozi inaoufanya.
“Ni bora hilo lifanyike hivi sasa kuliko hapo baadae, hatutaki kuongeza mvutano, lakini tuko tayari kwa hali yoyote kuidhibiti Iran dhidi ya mpango wake,”amesema Netanyahu
Aidha, Israel imekuwa ikirudia mara kwa mara kuonya kuwa haiwezi kuvumilia uwepo wa kudumu wa majeshi ya Iran katika nchi jirani ya Syria.
Hata hivyo, Iran ni mshirika muhimu wa Rais wa Syria Bashar Assad, na imekuwa ikitoa misaada muhimu ya kijeshi kwa majeshi ya Assad.