Kiongozi wa upinzani nchini Urusi, Alexei Navalny na watu wengine 200 wamekamatwa na polisi katika maandamano ya nchi nzima ya kupinga kuapishwa kwa rais Vladimir Putin.

Navalny alizuiwa kushiriki kampeni za uchaguzi mkuu wa rais wa nchi hiyo uliofanyika Machi mwaka huu. hivyo kudai kuwa hakutendewa haki.

Aidha, Kukamatwa kwa kiongozi huyo kumetokana na kuwa na ushawishi mkubwa wa watu waliojitokeza katika maandamano hayo ya kupinga kuapishwa kwa rais wa nchi hiyo.

Hata hivyo, kabla ya kuanza maandamano hayo, wafuasi wa rais Putin nao waliandamana katika uwanja uliopo katikati ya mji mkuu wa Urusi, walipokuwa wamekusanyika wafuasi wa Navalny, kulingana na taarifa za waandishi habari wa AFP.

 

Simba yatamba kukusanya pointi tatu kwa Ndanda FC
Tuzo za Nobel zayeyuka kwa kashfa ya ngono