Mwanamuziki nguli kutoka nchini Marekani Jennifer Lopez ametangaza uchumba wake na mwigizaji Ben Affleck miaka 19 baada ya wapenzi  hao kusitisha harusi yao na kutengana kwa mara ya kwanza.

Lopez ambaye ni mwimbaji na mwigizaji maarufu, 52, alishiriki habari hiyo na mashabiki wake kupitia jarida lake maalum la ‘On The JLo’ akionesha barua pepe hiyo na kipande kidogo cha video yake kikimuonyesha akivutiwa na pete ya uchumba yenye mawe ya kijani kwenye kidole chake.

Video hiyo pia ilielekezwa usoni mwake na kisha  kumwonesha akionekana kufuta machozi, kabla ya kusema “Wewe ni mkamilifu.”

Lopez alitilia mkazo taarifa hiyo kwa kuchapisha kupitia ukurasa wake maalum wa matandao wa twitter na Instagram, ambapo aliwahimiza wafuasi kujisajili katika jarida lake ili kuwa karibu na taarifa zaidi.

Habari hizo zinakuja mwaka mmoja baada ya wawili hao kuanzisha tena penzi hilo hadharani baada ya takriban miongo miwili kupita.

Lopez na Affleck walianza uchumba mnamo Julai 2002, na wakatangaza kuchumbiana mnamo Novemba mwaka huo walipaswa kufunga ndoa Septemba iliyofuata lakini waliahirisha siku za harusi kabla ya sherehe na Mnamo Januari 2004, waliuvunja uchumba wao na kutengana kabisa.

“Mimi na Ben tuliachana wakati qmbao niliwaza kwamba tunajitolea milele, ilikuwa ni huzuni yangu ya kwanza ya moyo, nilihisi kama moyo wangu umetolewa nje ya kifua changu,” Lopez aliandika kupitia Page Six mnamo mwaka wa 2014.

Siku tatu tu baada ya kuahirishwa kwa harusi hiyo, Lopez alianza uhusiano mpya wa kimapenzi na mwimbaji  maarufu wa nchini Marekani Marc Anthony na ilipofika Juni mwaka huo huo wa 2004 wawili hao walifunga ndoa.

Lopez alithibitisha kurudiana na Affleck kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram  baada ya siku yake ya kuzaliwa akitimiza umri wa miaka 52, alipochapisha picha yake akimbusu mwigizaji huyo wakiwa kwenye boti binafsi.

“Huwezi kufikiria kitu kama hicho kinaweza kutokea,” Lopez alimwambia Ellen DeGeneres kuhusu uhusiano huo. “Ni jambo zuri.”

Punde baada ya kuacha hapo awali Affleck naye alimuoa mwigizaji Jennifer Garner, ambaye alizaa naye watoto watatu  ambao ni Violet, 16, Seraphina, 13, na Samuel, 10. na baadae mwaka  2018 walitalikiana wakiwa wamedumu kwa muda wa miaka 13 ya ndoa.

Lopez yeye alikuwa ameolewa na Marc Anthony ambapo walidumu kwa muda wa miaka 10. Walitalikiana mwaka 2014, na walibarikiwa watoto wawili mapacha Emme na Max, 14.

Kabla ya heka heka za Lopez na wapenzi wake wawili Affleck na Mac anton, ikumbukwe huko nyuma Jenifer Lopez pia aliolewa na Ojani Noa hii ilikuwa mnamo 1997 hadi 1998, na Cris Judd kutoka 2001 hadi 2003.

Mgosi: Pablo atavunja rekodi Simba SC
Uganda: Wanaosema Spika Oulanyah aliuwawa kwa sumu wasakwa