Polisi nchini Uganda wametishia kuwakamata watu wanaodai kwamba aliyekuwa spika wa nchi hiyo Jacob Oulanyah aliuawa kwa kupewa sumu.

Oulanyah aliaga dunia March tarehe 19 2022 akipokea matibabu nchini Marekani baada ya kutibiwa katika hospitali tofauti nchini Uganda na Kenya.

Kufuatia kifo chake, uvumi ulienea nchini Uganda kwamba Oulanyah alifariki kutokana na madhara ya sumu aliyopewa na kwamba sumu hiyo ilikuwa ya mda mrefu mwilini kabla ya kusababisha kifo.

Baada ya kifo cha Oulanyah, Rais wa Uganda Yoweri Museveni alisema ametoa amri kwa polisi kufuatilia wanaondika kwenye mitandao ya kijamii kuwa Jacob Oulanya alifariki baada ya kupewa sumu, na kuwakamata wanaotoa madai hayo ili watoe ufafanuzi na kueleza polisi kile wanachokijua.

Hata hivyo wakati wa mazishi yake, baba wa OulanyahNathan L’Okori, kupitia kwa mkalimani, alisema kwa lugha ya Luo kwamba mtoto wake alimwambia kuwa amepewa sumu na ndio chanzo cha safari ya mwisho ya uhai wake.

“Nataka walio hapa wote kujua kwamba Oulanyah alipewa sumu. Aliniambia mwenyewe kwamba alipewa sumu. Alifanyiwa upasuaji. Madakatari walijaribu kukabiliana na sumu hiyo lakini tayari ilikuwa imesambaa mwilini. Wakati alisafirishwa kwa ndege kupata matibabu Marekani, alikuwa katika hali mbaya ambayo hangepona.” alisema baba wa Oulanya.

Mnamo mwezi Agosti mwaka uliopita, gazeti la Observor la nchini Uganda, liliripoti kwamba Rais Yoweri Museveni alikuwa ameagiza timu maalum ya usalama kuchunguza sababu zilizokuwa zikipelekea afya ya Spika Jcaob Oulanyah, ikiwemo madai ya kupewa sumu.

Kwa upande wake Naibu mwenyekiti wa chama kinachotawala cha National resistance movement NRM, Godfrey Kiwanda, ameambia radio moja ya nchini Uganda siku ya Jumapili asubuhi April 9, kwamba Jacob Oulanyah, alimwambia alipewa Sumu baada ya kushinda uchaguzi wa kiti cha Spika Mwezi May mwaka uliopita.

” Aliniambia alikuwa amepewa sumu na kwamba tukio hilo lilifanyika mda mfupi baada ya kushinda uchaguzi wa kiti cha spika, mwezi May mwaka uliopita 2021. Oulanyah mwenyewe akiniambia kwamba alipewa sumu. Hakujua ni wapi alipewa sumu hiyo wala hakuiambia aliyempa sumu. Sasa haya madai ya aliyekuwa spika kupewa sumu hayakuanza a familia yake. Yalianza na Oulanyah mwenyewe akiwa hai. Na siwezi kunyamaza kusema ninachokijua. Hata niliambia baadhi ya watu wakati Oulanyah alikuwa bado hai.”

Kutoka Nchini Tanzania Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson alishiriki mazishi ya Oulanyah akiiwkailisha nchi ya Tanzania.

Dkt. Tulia Ackson katika ibada ya maziko ya Jacob Oulanya

Wakati wa mazishi ya Oulanyah, jumamosi April 8 2022, waziri wa afya wa Uganda Dr. Jane Ruth Aceng, alisema kwamba Oulanyah alifariki baada ya viuongo muhimu mwilini kukosa kufanya kazi. Moyo ulishindwa kufanya kazi, mapafu, ini na kulikuwa na maambukizi katika sehemu kadhaa za mwil na Alifariki nchini Marekani.

J-Lo arudiana na Mwanaume aliyemuacha miaka 19 iliyopita
Wasichana takribani 20 huambukizwa VVU kila wiki Kenya