Jaji Mkuu wa Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Hamis Juma amewataka wanasheria wa serikali ambao wapo katika  utumishi wa umma, kuhakikisha kwamba sheria wanazozisimamia lazima zikidhi matarajio ya maendeleo na ustawi wa wananchi maskini.

Ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa wanasheria walio katika utumishi wa umma unaofanyika katika Chuo cha Mipango.

“Wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na kupitia katiba ya Jamhuri ya Muungano, Serikali, Bunge na Mahakama, zinapata mamlaka zao kutoka kwa wananchi. Wanasheria katika sekta ya umma hakikisheni kuwa sheria  zinalenga ustawi wa wananchi,”amesema Prof. Juma

Aidha, Jaji Mkuu amebainisha katika mkutano huo unaowakutanisha mawakili wa serikali 900 kutoka Wizara mbalimbali,  Idara , Taasisi za Serikali na Mamlaka ya Serikali za Mitaa, kwamba portfolio pana ya Wizara ya Katiba na Sheria inampa Waziri upeo mpana wa kuhakikisha kuwa Sheria za Tanzanbia zinalenga katika ustawi wa wananchi ambao wengi wao ni wenye hali duni ya maisha.

Hata hivyo, Jaji Mkuu Prof. Juma ameongeza kuwa sheria hizo lazima ziwasaidie wananchi maskini kunufaika na Malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025.

 

 

Video: JPM afunguka kuhusu sakata la Makontena ya Makonda
Wizara ya afya yatuma mtaalum kuchunguza mwili wa mwanafunzi aliyeuawa Bukoba