Msajili wa vyama vya Siasa Nchini, Jaji Francis Mutungi amevitaka vyama vya siasa nchini kuweka pembeni tofauti zao na migogoro iliyopo ili kuweza kutoa fursa kwa wajumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini kutoa maoni yao kwa ajili ya maendeleo nchini.
Ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati wa ufunguzi wa kikao cha Baraza la vyama hivyo, ambapo amesema kuwa anafahamu kuna migogoro inayoendelea ndani ya baadhi ya vyama.
Amesema kuwa anapendekeza wajumbe wote wa vyama vyote washiriki hata kama ndani ya baadhi ya vyama kuna migogoro.
“Nafahamu kuna baadhi ya vyama vina migogoro ikiwamo Chama cha Wananchi (CUF), lakini hapa mtawaona watu wengine tofauti ambao wanasuguana,”amesema Mutungi
-
Video: Marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa yaiva
-
Video: Makamu wa Rais akagua mifereji Jijini Dar
-
Mambosasa akanusha agizo la vimini na viduku
Hata hivyo, ameongeza kuwa Baraza hilo limetokana na vyama 19, vya siasa vilivyo sajiliwa ambapo kunatakiwa kuwepo wajumbe 38 wawili kila chama.