Jambazi sugu wa Ufaransa, Redoine Faid aliyetoroka jela kwa kutumia helkopta, Julai mwaka huu amekamatwa tena.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi la Ufaransa, Redoine ambaye alikuwa mtu anayetafutwa zaidi nchini humo amekamatwa mapema leo nchini humo.
Alitoroka jela alipokuwa anatumikia kifungo chake, baada ya watu wenye silaha nzito kuvamia jela hiyo iliyoko Kaskazini mwa jiji la Paris. Watu hao walimchukua na kuondoka naye kwa kutumia helkopta ambayo walikuwa wameiteka.
Mhalifu huyo alikamatwa kwa mara ya kwanza mwaka 1998 kwa kosa la kufanya unyang’anyi, mwaka 2009 alijisalimisha na kutangaza kubadilika kitabia.
Hata hivyo, alikamatwa tena akihusishwa na tukio la unyang’anyi ambalo lilisababisha kifo cha askari wa kike wa jeshi la polisi mwaka 2010 na alihukumiwa kifungo cha miaka 25 jela, lakini alitoroka tena Julai mwaka huu.
Waziri wa Sheria wa Ufaransa, Nicole Belloubet aliwaambia waandishi wa habari kuwa Serikali itahakikisha hatoroki tena.
“Tutamuweka kwenye jela yenye ulinzi wa hali ya juu ambako atakuwa akiangaliwa kwa ukaribu zaidi,” alisema.
Redoine Faid mwenye umri wa miaka 46, alianza kuendesha kundi la kihalifu mwaka 1990, kundi ambalo lilikuwa linajihusisha na unyang’anyi wa kutumia silaha.
Mwaka 2009, alitoa kitabu kinachohusu maisha yake, ambapo kupitia kitabu hicho alieleza kuwa filamu za ujambazi ndizo zilizomvutia kujiingiza kwenye uhalifu na kwamba amekuwa akitumia mbinu za filamu hizo kutekeleza mipango yake.
Alizitaja filamu hizo kuwa ni pamoja na Al Pacino thriller Scarface