Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani 2023, Kitaifa yanafanyika Mkoani Morogoro hii leo Desemba 1, 2023 katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Morogoro.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima, akiongeza na vyombo vya Habari alisema Mgeni rasmi wa Maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa ambapo Kauli mbiu ya mwaka huu ni “Jamii iongoze kutokomeza UKIMWI.”

Wiki ya maadhimishoya siku ya UKIMWI Duniani ilizinduliwa Novemba 24, 2023 ikiongozwa na mfululizo wa matukio na utoaji wa huduma mbalimbali za wataalamu zikiwemo upimaji wa VVU, uchunguzi wa magonjwa sugu yasiyoambukiza (Kisukari, Shinikizo la damu, uchunguzi wa Saratani ya Mlango wa kizazi, lishe), elimu na uchunguzi wa Kifua Kikuu, uchangiaji damu na huduma ya kwanza.

Matukio yaliyofanyika ndani ya Wiki ya Maadhimisho ni pamoja na Mbio za nyika (ATF Marathon) na mbio hizo zililenga kuhamasisha na kuutangaza mfuko wa udhamini wa kudhibiti UKIMWI – ATF.

TAKUKURU kuongeza kasi ufuatiliaji miradi ya maendeleo
Ali Maaloul: Tunafahamu ubora na udhaifu wao