Timotheo Mathayo – Dar es Salaam.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amezitaka kampuni za Bima nchini kuendelea kutoa elimu kwa umma ili kuwajengea  uwezo Wananchi kufahamu faida ya kuwa na bima zitakazowasaidia katika nyanja mbalimbali ikiwemo makazi na usafiri.

Dkt. Biteko, ameyasema hayo wakati akizungumza na Watendaji wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania – TIRA, Jijini Dar es Salaam na kudai kuwa ili kuendelea kukuza uchumi wa Taifa kwa ujumla, kampuni za Bima zinatakiwa kutunza fedha zake kwenye Benki za ndani ya nchi jambo ambalo litachochea  maendeleo.

Kwa upande wake, Katibu wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar na Katibu Mkuu Kiongozi Mha. Zena Ahmed Said ambaye pia ni Balozi wa Bima Tanzania amesema Mamlaka inaendelea na mkakati wa kutoa elimu kwa umma kwa kushirikiana na mashirika ya Serikali na Sekta Binafsi.

Amesema, lengo ni kuwafikia  watanzania asilimia 80 wenye zaidi ya umri wa miaka 18 ifikapo mwaka 2030 pia  Mamlaka inaendelea na hatua ya  kuhamasisha Wizara na Taasisi za Serikali ziweke Bima kwenye miradi inayotekelezwa katika Sekta hizo.

Cedrick Kaze kumfunga paka kengele?
Wizara yalaani tukio kuteswa kwa Mtoto, wahusika wasakwa