Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe ameonya kwamba wawekezaji katika bara la Afrika wanatakiwa kuchukua tahadhari dhidi ya kuzibebesha mzigo mkubwa wa madeni nchi za Kiafrika.
Onyo hilo la Shinzo Abe limeilenga zaidi China ambayo sera yake ya ujenzi wa Miundombinu ya reli na barabara imekuwa ikikosolewa kwamba inaziangamiza nchi masikini kwa kuzibebesha madeni makubwa.
Akizungumza na waandishi habari mara baada ya kumalizika kwa mkutano wenye dhamira ya kuendeleza ustawi wa bara la Afrika uliofanyika nje kidogo ya jiji la Tokyo, Abe amesisitiza kuwa nchi za kundi la G20 ikiwemo China zimejitolea katika mpango wa kuyadhibiti madeni ili kuzisaidia nchi za Afrika suala la mzigo wa madeni linapaswa kuzingatiwa na kudhibitiwa yasipite kiwango.