Rais wa zamani wa Sierra Leone, Ernest Bai Koroma ameripoti Kituo cha Polisi katika mji Mkuu wa Nchi hiyo Freetown ili kuhojiwa kuhusiana na kile Serikali ilichodai ni kutokana na jaribio la mapinduzi la mwishoni mwa mwezi Novemba, 2023.

Koroma ambaye aliiongoza nchi hiyo ya Afrika Magharibi kwa miaka 11 hadi 2018, aliwasili katika idara upelelezi wa jinai akiwa chini ya ulinzi mkali wa Polisi na kusindikizwa na Jeshi baada ya kutakiwa kuwasili hapo ndani ya kipindi cha saa 24.

Siku ya tukio, Washambuliaji waliokuwa na silaha walivamia ghala ya silaha ya Jeshi, kambi mbili, Magereza mawili na vituo viwili vya Polisi ambapo walipambana na vikosi vya usalama nyakati za subuhi Novemba 26, 2023.

Waziri wa Habari wa Sierra Leone, Chernor Bah akizungumzia tikio hilo alisema wakati wa mapigano hayo, watu 21 waliuawa na tangu wakati huo watu 71 wamekamatwa na uchunguzi kuhusu tulio hilo bado unaendelea ili kubaini ukweli.

Magari ya kifahari yatumika usafirishaji Dawa za kulevya
Endeleeni kutoa maeneo Miradi ya Umeme iwafikie - Kapinga