Je unafahamu faida mbalimbali za kudeka, kwani wataalamu mbalimbali wa masuala ya afya wanashauri mtu anatakiwa kudeka mara kwa mara kwa mpenzi wake kutokana na matokeo mazuri kwenye afya yake.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Toronto uliochapishwa mwaka 2014 kwenye jarida la Archives of Sexual Behaviour unataja faida mbalimbali za kudeka kwa mtoto na mtu mzima.
Ambapo unaambiwa kwamba kwa watoto wadogo kudeka huwasaidia katika kuimarisha mzunguko wao wa usingizi, lakini pia huwaondolea maumivu mbalimbali ya mwili, huwakinga dhidi ya magonjwa hasa mafua pamoja na kuongeza upendo zaidi kwa wazazi wao.
Na kwa watu wazima kudeka husaidia mambo yafuatayo.
- Husaidia kuongeza homoni za mapenzi yaani Oxytocin ambayo huamsha hamu ya kushiriki tendo.
- Huimarisha afya ya moyo
- Huimarisha mahusiano ya kimapenzi
- Hupunguza shinikizo la damu
- Huboresha usingizi
- Huimarisha mfumo wa mwili katika kupambana msongo wa mawazo.
Wapo wanaopenda wapenzi wanaodeka lakini pia wapo wasiopenda wapenzi wanaodeka kwa madai kuwa mara nyingi wanakuwa na tabia za kitoto.
Lakini pia kudeka ni malezi ya mtu, mara nyingi kudeka ni tabia inayofanywa zaidi na watu wenye maisha mazuri ya kifahari maana unapodeka unauhakika wa kupata kitu chochote unachokihitaji na kwa wakati, na tabia hii huanzia tangu unapokuwa mtoto kutoka kwa wazazi wako.
Walio wengi waliokumbana na maisha magumu ya shida na tabu kudeka si sehemu ya maisha yao, lakini pia suala jingine linalojitokeza hapa ni je unaweza kumdekea mpenzi uliyenaye sasa?
Tuandikie maoni yako hapa chini.