Mahakama ya Kikatiba nchini Congo DRC imesema kuwa kiongozi wa upinzani, Jean-Pierre Bemba, hana sifa ya kuwa rais wa nchi hiyo.
Kiongozi huyo amezuiwa kugombea nafasi ya uraisi katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Bemba, ambaye anatajwa kama mpiganaji wa zamani, aliyewahi pia kushika wadhifa wa makamu wa raisi nchini humo, amekosa sifa za kustahili kusimama na kugombea nafasi hiyo kutokana na sababu mojawapo inayotajwa kuwa ni hukumu iliyotolewa na mahakama ya Kimataifa ya Jinai kwa madai ya kuwahonga mashahidi.
Aidha, hivi karibuni Bemba aliachiwa huru katika kesi dhidi ya uhalifu wa kivita na mahakama baada ya kutumikia miaka kumi jela.
Hata hivyo, Jean-Pierre Bemba anatajwa kama mpinzani namba moja anayesumbua kichwa cha rais wa nchi hiyo, Joseph Kabila katika uchaguzi ujao