Mahakama ya Wilaya ya Tabora, imemhukumu kifungo cha maisha jela mkazi wa Kidatu “B” Kata ya Mtendeni mkoani humo, Hussein Mashibu (32) baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mtu mzima hadharani huku watu wakishuhudia kwa kumtuhumu kuwa ana mahusiano na mke wake.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Wilaya ya Tabora, Sigwa Mzige alisema mahakama imeona kifungo hicho kwa mshitakiwa kinastahili kwani alifanya unyama usioweza kuvumiliwa na jamii.

Mzige alisema, ushahidi uliotolewa umeonesha hauna shaka yoyote ukilinganisha na ushahidi uliotolewa na mtuhumiwa mwenyewe na daktari ambaye alithibitisha kutokana na vipimo vya aliyelawitiwa kupata michubuko na alipewa dawa ya misuli.

Wakili wa Serikali, Robert Kumwembehiyo kwamba mtuhumiwa alipatikana na kosa la kumlawiti mtu mzima (jina limehifadhiwa) Januari 30, mwaka jana katika maeneo ya Kidatu ‘B’ mkoani Tabora.

Mtuhumiwa alishitakiwa kwa makosa mawili ya kulawiti na kujeruhi kwa kumpiga na kitu kichwani na kumsababishia jeraha na makosa yote yanakwenda pamoja ikiwemo kulipa faini ya Sh milioni moja.

Picha: Rais Samia katika Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani
Washauriwa kuwashirikisha Wananchi utambuzi madai ya haki