Afisa mmoja wa Polisi nchini Uingereza David Carrick, mwenye umri wa miaka 48 amekiri kufanya makosa kutekeleza makosa 71 ya ubakaji dhidi ya wanawake 12 wakati akihudumu kama Polisi kati ya mwaka 2003 na 2020.

Carrick anadaiwa kuwatesa na kuwanyanyasa wanawake hao kwa miaka 17 licha ya kushtakiwa mara tisa kabla ya kukamatwa kwake mwaka wa 2021 wakati tuhuma za ubakaji na unyanyasaji wa nyumbani zilipoibuliwa dhidi yake.

Aidha, inaarifiwa kuwa Carrick alikuwa akikutana na wanawake hao waliobakwa kupitia tovuti za mapenzi na kuwafanya watumwa wake.

Afisa mmoja wa Polisi nchini Uingereza, David Carrick.

Idara ya polisi ya Met iliomba radhi kwa kushindwa kwake kumzuia Carrick ikisema alikuwa akiwatishia waathiriwa akisema hawataaminika wakimshtaki huku Kamishna Msaidizi wa polisi Barbara Gray akiwaomba radhi waathiriwa akisema.

Alisema, “Tunasikitika sana kwamba kuweza kuendelea kutumia nafasi yake kama afisa wa polisi kunaweza kuongeza mateso ya waathiriwa wake. Tunajua walihisi hawawezi kujitokeza mapema kwa sababu aliwaambia hawataaminika.”

Desemba 2022, alikiri makosa mengine 43 ikiwa ni pamoja na makosa 20 ya ubakaji na aliwafanyia ukatili huo Wanawake 12 kati ya 2003 na 2020 wakati Carrick alikuwa akihudumu kama afisa wa dharura katika majengo ya Bunge na alisimamishwa kazi alipokamatwa Oktoba 2021, na atahukumiwa mnamo Februari 6, 2023.

Bernard Morrison aichokonoa Young Africans
Simba SC yarejea Dar, mashabiki waitwa Kwa Mkapa