Johansen Buberwa, Kyerwa – Kagera.
Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Zaituni Msofe amewata Askali wa Jeshi la Akiba kuendelea kuwa na uzalendo, uadilifu pamoja na kuisaidiaTaifa la Tanzania kupambana na vitendo vya uhalifu, hali itakayowasaidia kuleta maendeleo na uchumi.
Amesema hayo katika hafla ya kuhitimisha mafunzo ya Mgambo Wilayani humo yaliyofanyika kata ya Kikukuru Tarafa ya Mabila na kusema uzalendo na kulipenda Taifa ni jambo la msingi.
Amesema, “tumeongeza jeshi la Akiba ambapo tunatumaini kwamba mtatusaidia katika kupunguza vitendo vya uhalifu tunategemea mtaungana na wenzenu ambao wamesha maliza mafunzo kwa muda mrefu kama majeshi mengine kutusaidia Wilaya Kyerwa ibaki salama kwa amani na utulivu.”
Awali, Kaimu mshari wa Mgambo Wilaya, SSGT. Deomedes Rupia alisema kuwa mafunzo ya awali ya akiba yalianza Juni 5, 2023 kwa muda wa majuma 28 yakiwa na jumla ya wahitimu 72 wakiume 70 na wakike wawili na hadi siku ya kuhitimu idadi yao ni jumla ni 58 wakiume 56 na wakike 2 kutona na sababu mbalimbali ikiwemo utovu wa nidhamu na kutokidhi vigezo.
Kwa upande wao Baadhi ya wahitimu wa mafunzo hayo, akiwemo Devotha Tumwamini na Pastory wameishuru Serikali kwa kupata mafunzo hayo huku akiomba kupewa kipaumbele cha ajira kwa watoto wa kike ambao wamesaulika, ikiwemo ile ya usimamizi wa mithiani na kuunganishwa na Suma JKT.