Mahakama ya Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani, imemuhukumu kifungo cha maisha jela aliyekuwa Mwalimu wa Shule ya Msingi St. Methew iliyopo Kongowe, Livingstone Kyarwenda (40), baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti Mwanafunzi wake (9).

Kyarwenda, anadaiwa kumlawiti Mwanafunzi wa kiume aliyekuwa anasoma darasa la nne katika vyoo vilivyopo Shuleni hapo.

Uamuzi huo, umetolewa leo Novemba 29, 2023 na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Herieth Mwalola kufuatia kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutolewa hukumu.

Viongozi wa Dini wajengeni Vijana kimaadili - Dkt. Yonazi
Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Novemba 30, 2023