Jeshi la Polisi Nchini limesema kuwa hali ya usalama Wilayani Kibiti iko safi hivyo mtu yeyote anayetaka kwenda kuishi na kufanya shughuli zake huko ruksa kwakuwa kwa sasa jeshi hilo limeimarisha hali ya kiusalama hivyo wananchi hawapaswi kuhofia chochote.
Hayo yamesemwa na Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Barnabas Mwakalukwa, ambapo amesema kuwa hali ya usalama katika Wilaya za Kibiti, Rufiji na Mkuranga imeimarishwa sana hivyo Watanzania wanaweza kwenda kufanya shughuli zao huko bila woga.
ACP Mwakalukwa amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa Kanda Maalum katika eneo hilo, matukio ya uhalifu yamepungua na jeshi la Polisi limeweza kuwadhibiti watu wote waliokuwa wanajihusisha uhalifu.
“Zile taarifa kuwa sasa hivi eka 3,000 za ardhi Kibiti zinauzwa kwa sh. 1000 na hakuna mtu anayekwenda Kibiti si za kweli, hivi sasa hali ni shwari Kibiti anayetaka kwenda na aende hata mimi nitakwenda huko,”amesema Mwakalukwa.
-
IGP Sirro aanza kulisuka upya Jeshi la Polisi
-
Video: Jeshi la Polisi Dar lawataka wahalifu kujisalimisha
Hata hivyo, ameongeza kuwa kwa sasa anampango wa kwenda kuzitembelea wilaya za Kibiti,Mkuranga na Mafia hivyo amesisitiza kwa Mtanzania yeyote anayetaka kwenda huko kufanya shughuli zake aende bila hofu.