Jeshi la polisi Mkoani Pwani linawashikilia watu 20 kwa kosa la kuhusika na uuzaji wa dawa mbalimbali za kulevya ikiwemo heroin, mirungi na bangi . pia Jeshi hilo limekamata nyara za Serikali ,meno ya tembo sita thamani yake mil.98.100 na vipande 56 vya ngozi ya mbalawa .
Aidha, Jeshi hilo limefanikiwa kukamata magunia ya bangi 28, puli 270 ,heroin kete 700 ,lita 522 za pombe ya moshi (gongo) na mitambo saba ya kutengenezea pombe hiyo,misokoto 52 ,kete 2,853 na mirungi milaa 94 .
Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Boniventure Mushongi amesema kuwa pia wamewakamata wahamiaji haramu 153 ambapo kati ya hao saba walikutwa wakisafirishwa kwenye gari namba T.568 CZ
“Katika operesheni hiyo tumekamata watu 15 ambao wamekiri kujihusisha na matukio ya uporaji na mauaji kwenye matukio mbalimbali mkoani hapo,”amesema Mushongi.
Hata hivyo ,Kamanda Mushongi, amesema mafanikio hayo yametokana na operesheni iliyofanyika ndani ya wiki mbili baada ya kutokea tukio la mauaji ya aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Liwale Ephraim Mfingi Mbaga (54).