Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ( Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Jennista Mhagama amewataka vijana kujiepusha na madawa ya kulevya ili utekelezaji wa dhana ya Tanzania ya viwanda ilete ajira kwa vijana wenye nguvu
Ameyasema hayo Jijini Arusha wakati akifunga mkutano mkuu wa 9 wa wadau wa mfuko wa hifadhi ya watumishi wa Serikali za mitaa, LAPF uliohudhuriwa na wadau wa mfuko huo
Amesema kuwa kwa sasa Serikali imedhamiria kuwainua idadi kubwa ya vijana waliona ujuzi mdogo kwa kuwajenge uwezo kupitia mafunzo mbalimbali katika vyuo vilivyopo nchini
”Udhibiti mkubwa wa madawa ya kulevya unahitajika kwa vijana wetu ili kutengeneza taifa lenye nguvu ya kufanya kazi ”amesema Mhagama.
Aidha, ameongeza kuwa asilimia kubwa ya watanzania hawana ujuzi wa kutosha hivyo basi Serikali ya awamu ya 5 imejipanga ipasavyo kuhakikisha vijana wanapata ajira kupitia viwanda
Hata hivyo ameupongeza mfuko wa LAPF kwa kazi nzuri wanayofanya huku akiitaka mifuko yote ya kijamii hapa nchini ihakikishe kuwa ifikapo 2025 inakuwa na wanachama wengi zaidi

Jeshi la Polisi mkoa wa Pwani lawashikilia watu 30 kwa tuhuma za dawa za kulevya
Waajiri watakiwa kuwasilisha taarifa za wafanyakazi wao