Siku kadhaa baada ya waziri Mkuu mstaafu, Fredirick Sumaye kudai kuwa ameamua kuondoka CCM kwa madai kuwa viongozi wa chama hicho hawauoni umuhimu wake na kutomhusisha na baadhi ya mambo ya serikali, rais Jakaya Kikwete ameyatolea majibu.

Katika majibu yake, Rais Kikwete ameeleza kuwa kiongozi anayetoka madarakani hawezi kulazimisha kuombwa ushauri na kiongozi aliyeko madarakani. Alisema Rais yeyote huwa amekamilika kutokana na timu ya watu wake wanaomshauri kuhusu mambo mbalimbali lakini anaweza kuomba ushauri kwa kiongozi aliyetoka madarakani pale anapoona inafaa na sio lazima.

“Huwezi kulalamika kuwa huombwi ushauri,” alisema rais Kikwete na kuongeza kuwa yeye anamalizi muda wake wa uongozi na kustaafu na kwamba kama rais anayekuja ataona ni jambo muafaka kuomba ushauri atachangia kwa kadri ya uwezo wake lakini kiongozi yeyote aliyestaafu hawezi kulazimisha kuombwa ushauri.

 

Dk. Slaa Ajibu Alikotoa Fedha Za Kugharamia Mkutano Wake Na Matangazo
Askofu Kilaini Amshangaa Dk Slaa, Sumaye Naye Anena