Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa anapenda kuendelea kufanya shughuli zinazosaidia kuleta maendeleo kwa watu na jamii.
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam, wakati alipokuwa  akizindua Taasisi yake ya Jakaya Kikwete (Jakaya Mrisho Kikwete Foundation)  amesema kuwa kwa muda mrefu amekua akipenda na kujihusisha na shughuli mbalimbali za maendeleo ya watu na hivyo Taasisi yake itamsaidia katika kufikia malengo yake.
“Nimetumia muda wangu kwa ajili ya maendeleo ya watu, baada ya shule, nilikitumikia Chama cha Mapinduzi(CCM), nilitumikia Jeshi na baadae Serikali, kwangu Taasisi hii imekuwa chombo kitakachonisaidia kuendeleza maono yangu na kutimiza ndoto zangu katika kuendelea kusaidia watu” amesema Dkt. Kikwete.
 Amesema kuwa Taasisi hiyo imejikita kusaidia jamii katika maeneo makubwa manne, maendeleo ya jamii  hasa katika kujikita kuondoa umaskini, mabadiliko ya hali ya nchi na kilimo  kwa wakulima wadogo.
Hata hivyo, Maeneo mengine ambayo Taasisi hiyo inajihusisha nayo ni kutoa elimu kwa  vijana ili  kukuza vipaji vyao na kuwapa mafunzo kuhusu uongozi bora, usawa wa kijinsia na namna ambavyo Serikali inavyotoa huduma kwa wananchi.

Video: Makonda atangaza vita nyingine, “hawa ni halali yangu”
Serikali kuanza kuuza huduma zitolewazo na Wizara