Hatimaye Beki kutoka Kenya Joash Onyango Achieng amefunguka sakata lake la kutaka kuvunjiwa mkataba wake Simba SC, na kupelekea taharuki kubwa kwa Mashabiki na Wanachama wa Msimbazi kwa kipindi cha mwezi uliopita.

Onyango amefunguka juu ya sakata hilo baada ya mchezo dhidi ya Tanzania Prisons jana Jumatano (Septemba 14), jijini Mbeya ambapo amekiri alishinikiza kuvunjwa kwa mkataba wake.

Amesema sababu kubwa ya kufanya maamuzi hayo hadi kubisha hodi kwenye Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF, ilitokana na mwenendo ambao hakuuona kuwa na mustakabali mzuri katika soka lake akiwa Simba SC.

Sababu nyingine iliyotajwa na Onyango ni mipango ya Kocha Zoran Maki ambayo ilithibitisha kumuweka pembeni na hakuona sababu ya kuendelea kuwepo klabuni hapo.

“Ni kweli niliomba kuondoka Simba SC kwa sababu kocha aliyekuwa amekuja alisema sipo katika mipango yake.”

“Kwa Sasa Mimi Ni mchezaji wa Simba nitaendelea kuwepo na ninawaomba mashabiki wazidi kutuombea na waje kwa wingi uwanjani” amesema Joash Onyango

Kwa mara ya kwanza Onyango Jana Jumanne (Septemba 14) aliitumikia Simba SC tangu kuanza kwa msimu huu 2022/23, akichukua nafasi ya Henock Inonga Baka.

Juma Mgunda: Mashabiki Simba SC waniheshimu
Henock Inonga Baka akumbukwa DR Congo