Beki wa Kati wa Klabu ya Simba SC Henock Inonga Baka ametajwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya DR Congo kitakachopambana katika michezo ya kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’ dhidi ya Mauritania mwezi huu.

Hii inakuwa mara ya kwanza kwa Beki huyo kutajwa kwenye kikosi cha DR Congo, tangu alipojiunga na Simba SC mwanzoni mwa msimu uliopita ‘2021/22’ akitokea Daring Club Motema Pembe.

Inonga pia anakuwa mchezaji pekee anayecheza Ligi Kuu Tanzania Bara kutajwa kwenye kikosi cha DR Congo katika kipindi hiki cha kuelekea michezo ya kuwania kufuzu Fainali za AFCON 2023.

Kikosi cha wachezaji 28 kilichotajwa na Kocha Sébastien Desabre

DR Congo itaanzia nyumbani kupambana dhidi ya Mauritania katika mchezo wa mzunguuko watatu wa Kundi I, baadae mwezi huu, na kisha itakwenda Mauritania kwa ajili ya mchezo wa Mzunguuko watano.

Hadi sasa DR Congo inaburuza mkia wa Kundi I, kufuatia kupoteza michezo miwili iliyopita, ikifungwa dhidi ya Gabon 1-0 na kisha ikapoteza dhidi ya Sudan 2-1.

Joash Onyango afunguka sakata lake Simba SC
Haji Manara apunguziwa adhabu TFF