Beki wa Kati wa Young Africans Dickson Job amesema wapo tayari kwa mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Fainali, Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya USM Alger.

Young Africans itakuwa nyumbani kesho Jumapili (Mei 28) katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, kisha watakwenda Algeria kwa ajili ya mchezo wa Mkondo wa Pili, utakaopigwa Juni 03.

Job ameweka wazi utayari wa kikosi cha Young Africans alipozungumza na katika Mkutano na Waandishi wa Habari leo Jumamosi (Mei 27) Mchana, katika Ukumbi wa Mikutano wa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Beki huyo amesema tayari Benchi la Ufundi limekamilisha Programu ya kuwaandaa wao kama Wachezaji, ambao wana jukumu la kuipambania Young Africans katika mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu kubwa na Wadau wa Soka katika Bara zima la Afrika.

“Tayari Walimu Wameshatupa Maelekezo ya nini kifanyike ndani ya Uwanja , Kazi Imebaki Kwetu Wachezaji Kwenda kupambana Uwanjani Ili tushinde Mchezo huu ”

“Watanzania waondoe uoga, nawaomba wajitokeze kwa wingi siku ya kesho na kushangilia kwa dakika zote. Vijana wao tuko tayari kwa ajili ya kupambana kuwapa furaha.” Amesema Job

Young Africans itatakiwa kusaka ushindi mkubwa katika mchezo wa kesho ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kuelekea mchezo wa Mkondo wa Pili ambao utachezwa mbele ya Mashabiki wa USM Algier, wanasifika kwa hamasa ya kuipa nguvu timu yao inapocheza nyumbani.

Kocha USMA aweka wazi mfumo wake
Mbunifu jezi za Young Africans afunguka