Kocha Mkuu wa USM Alger Abdelhak Benchikha amesema kikosi chake kitapambana kwa kushambulia katika mchezo wa ugenini ambao unakwenda kuwakutanisha na Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans.

USM Algier ambao wapo Dar es salaam tangu jana Ijumaa (Mei 26) Alfajiri, watacheza mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Fainali, Kombe la Shirikisho Barani Afrika kesho Jumapili (Mei 28), katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, huku mchezo wa Mkondo wa Pili ukitarajiwa kuchezwa nchini kwao Algeria Juni 03.

Kocha Benchikha ameanika mipango ya kupambana kwa kushambulia alipozungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika leo Jumamosi (Mei 27) mchana, katika Ukumbi wa Mikutano wa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kocha huyo amesema: “Katika mchezo wa kesho dhidi ya Young Africans tutacheza kwa kushambulia na wala hawatakaa nyuma kama wachezaji wa Tenis, Hatuna sababu ya kucheza kama tupo ugenini kwa kuwa fainali haina nyumbani wala ugenini.”

Kuhusu umahiri wa Mshambuliaji hatari wa Young Africans Fiston Kalala Mayele, Kocha Benchikha amesema: “Kila wakati ni Mayele, Sisi hatuendi kumkaba Mayele, mfumo ndio utamkaba, hivyo tutapambana kuhakikisha kuwa tunacheza vizuri na tunapata matokeo.”

Young Africans itatakiwa kusaka ushindi mkubwa katika mchezo wa kesho ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kuelekea mchezo wa Mkondo wa Pili ambao utachezwa mbele ya Mashabiki wa USM Algier, wanasifika kwa hamasa ya kuipa nguvu timu yao inapocheza nyumbani.

Rais Kenya awajibu wanaokataa kulipa mkopo
Dickson Job: Mashabiki msiogope njooni kwa wingi