Hatimaye Mwamba wa Kaskazini, Joh Makini ametoa neno kwa wale wanaodai kuwa amekuwa akibebwa kwenye muziki wake, licha kuteka mitaa na hits.

Rapa huyo Mweusi ambaye hudai kuwa hajui kutoa nyimbo bali hutoa ‘hits’, ametoa neno lake baada ya Young Killer kutema mstari unaomgusa kwenye wimbo wake mpya wa ‘Sinaga Swag’, “Wanasema Joh anabweba hadi nahisi ni ukweli.”

“Kwanza nashukuru Dulla wewe umeanza na ushahidi [wa hits ulizozitaja] kwahiyo umeshamaliza… kwa sababu hiyo Kamba ya mbeleko hiyo kutoka mwaka 2005 hadi 2015 basi hiyo Kamba ngumu,” Joh alifunguka kupitia Planet Bongo ya East Africa Radio.

Hata hivyo alisisitiza kuwa siku zote hapendi kutoa nafasi ya kuzungumzia mambo aliyoyaita ya kipuuzi katika mahojiano yake.

Naye Nikki wa Pili ambaye ni mdogo wake Joh aliamua kutolea ufafanuzi mashambulizi ya kubebwa yanayotolewa na baadhi ya wasanii akidai kuwa tatizo ni watu kumfahamu Joh Makini badala ya kuifahamu historia yake.

“Tatizo ninaloliona kwenye huo mstari kama huo… Kwa sababu Joh amefanya kazi kubwa sana. Wasanii hawa wadogo hawatakiwi tu kumjua Joh Makini, kumjua sio issue wanatakiwa kujua historia ya Joh Makini kwa sababu pale ndio kuna mafunzo mengi,” alisema Nikki.

Katika suala la kubebwa, Nikki wa Pili alieleza kuwa Muziki wa Joh Makini ni kama hela ndio sababu kila mtu anataka kuubeba.

Alama ya msingi ya kupigia mstari hapa ni historia ya Joh Makini. Huenda kama anavyosema Nikki wa Pili kwa waliokutana na Joh akiwa Dar na hits kadhaa ndio wanaopata shida.

Kwa shabiki wa Joh Makini aliyeanza kumfahamu tangu akiitwa ‘Rapture’ hata kabla ya kuachia ‘Hao’ kushiriki ‘Kama Kawa’ anaweza kurusha ngumi akisikia neno ‘anabebwa’.

 

 

 

Q Chief ataka sapoti ya Diamond, 'kumsainisha WCB'
Majaliwa azindua SACCOS ya Melinne, awataka viongozi kuwa wawazi