Msanii wa Bongo Fleva, Q Chillah, ambaye kwa sasa anafanya vizuri na video yake ya Sungura iliyoachiwa rasmi Dec 15, 2016,  video hiyo mpya iliongozwa na Director Justin Campos wa Afrika Kusini.

Q Chief hivi karibuni alitembelea ofisi za WCB na kufanya mazungumzo na uongozi wa label hiyo.

WCB ni label kubwa ya muziki nchini, ambayo ipo chini ya  Diamond Platnumz, huwenda ikamsaini msanii mkongwe wa muziki nchini Q Chief.

Akiongea katika kipindi cha Yaliyomo yamo cha Radio One Stereo Jumatano hii, Q Chief amedai hivi karibuni alikuwa kwenye mazungumzo la label kubwa ya muziki nchini Tanzania.

“Tayari nimenza kuyaa approach makampuni makubwa sana,” alisema Q Chief. “Kuna uwezokano nikasaini na mmoja ya wadogo zangu ambaye anafanya vizuri kuliko msanii yeyote hapa nchini,”

Aliongeza, “Lakini si nasaini kwa sababu mimi ni mjinga, nasaini kwa sababu nataka kuudhihirisha mimi ni Abubakar Katwila na hakunaga Abubakar Katwila mwingine,”.

 

JB: Millioni zimenitoka maandalizi kiu ya kisasi
Joh Makini amjibu Young Killer na wanaodai ‘anabebwa’