Nyota wa Filamu nchini, Jacob Steven maarufu kama ‘JB’ anazidi kufanya vizuri katika tasnia  ya uigizaji ambapo februari mwaka huu anatarajia kutoa kazi yake mpya ambayo itapendwa na wengi kutokana na uhalisia wa kazi hiyo ambapo amezungumzia mambo mbalimbali ya kujifunza katika maisha ya kila siku  ya Mtanzania.

JB licha ya kuwa muigizaji bora miongoni mwa nyota watano wa kiume kwa upande wa fani hiyo ya kucheza filamu pia ni mwandishi na mtayarishaji, anayetamba na kazi zake zilizofanya vizuri sokoni huko nyuma, ikiwemo, Illigal Sisters, Signature, Dereva tax,  D.N.A na nyingine.

Katika kuendelea kudhihirisha ubora wake na kazi zake, Jacob Steven JB mapema februari mwaka huu anatarajia kuachia tamthlia yake ya ‘Kiu ya Kisasi’ iliyomgharimu muda mwingi katika uandaaji wake.

JB alisema kwa sasa yupo katika makubaliano ya mwisho na vituo vya runinga ili kuweza kuanza kuionyesha tamthilia hiyo.

”Tamthilia imekamilika, mapema februari itakuwa ikioneshwa runingani ingawa bado sijajua ni runinga gani itaonyesha, hii itakuwa mfano kwa wasanii wengine kwa kuwa nimewekeza muda na fedha nyingi katika uandaaji wake,”  alisema JB.

 

Video: Tuhuma za rushwa ajira 600 Dangote, JPM ajibu mapigo...
Q Chief ataka sapoti ya Diamond, 'kumsainisha WCB'