Klabu ya Leicester City imekamilisha usajili wa mlinzi wa kati wa klabu ya West Bromwich Albion, Jonny Evans kwa mkataba wa miaka mitatu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 alikuwa akitakiwa na klabu za Arsenal na Manchester City mwaka jana lakini hakuweza kuhamia katika moja ya klabu hizo kutokana na ofa zao kukataliwa na West Brom na sasa amekubali kujiunga na na Leicester City baada ya West Brom kushuka daraja.
Evans anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na kocha Claude Puel wa Leicester baada ya usajili wa beki Ricardo Pereira kutoka katika klabu ya FC Porto.
Beki huyo raia wa Ireland ya Kaskazini ameichezea timu yake ya taifa jumla ya michezo 70.