Boris Johnson, Kiongozi aliyejiuzulu Uwaziri Mkuu wa Uingereza tangu aliposhikilia wadhifa huo mwaka 2019, na akiwa kiongozi wa kampeni ya Brexit 2016, amesema anasikitika kuiacha kazi bora ulimwenguni aliyokuwa akiipenda.

Kujiuzulu kwa Johnson kunafuatia uasi kutoka kwa chama chake cha Conservative, ambapo zaidi ya wabunge 50 walijiuzulu katika kipindi cha saa 36 kuanzia Julai 5, 2022, wakati Rishi Sunak, kansela wa hazina ya fedha, na Sajid Javid, katibu wa afya, walipojiondoa Serikalini.

Wengi wa waliojiuzulu walisema hawawezi tena kuendelea kuhudumu chini ya Johnson na wengine kumtaka ajiuzulu. Katika hotuba yake nje ya barabara ya 10 Downing,Johnson alisema ataendelea kuwa Waziri Mkuu hadi Kiongozi mpya atakapochaguliwa.

Boris Johnson kipindi akiwa Meya wa London wakati akijiandaa kuzungumza na vyombo vya habari mbele ya nyumba yake mjini London, Uingereza Februari 21, 2016. Uingereza ilikuwa ikijiandaa kupiga kura ya maoni kuhusu uanachama wa Umoja wa Ulaya Juni 23, 20216.

Akiwahutubia Waingereza, Johnson alisema “Nataka mjue jinsi ninavyohuzunika kuacha kazi bora zaidi ulimwenguni, lakini hayo ni mapumziko.”

Kwanini Johnson amejiuzulu:
Kujiuzulu kwa Boris kunafuatia kashfa na mabishano yaliyoikumba serikali yake hasa katika miezi iliyopita ambapo mwezi Aprili Johnson alipigwa faini kwa kuvunja sheria zake mwenyewe, kwa kuhudhuria na kuruhusu vyama kadhaa wakati wa kufungwa kwa Covid-19 nchini Uingereza.

Baadaye mwezi Juni, mshauri wa maadili wa Johnson, Christopher Geidt alijiuzulu akimtuhumu Waziri Mkuu kuvunja kanuni zake za uwaziri tukio lililofuatiwa na Wahafidhina walipoteza chaguzi mbili muhimu za marudio kwa kura nyingi, ikionyesha kwamba mamlaka ya chama hicho yalikuwa yakipungua kiusalama.

Boris Johnson akielekea kutoa hotuba yake ya kujiuzulu Julai 7, 2022 katika eneo la barabara ya 10 Downing jijini London Uingereza.

Hata hivyo, mwishoni mwa Juni wakati Chris Pincher naibu mkuu wa chama cha Conservative alijiuzulu baada ya kudaiwa kuwabembeleza wageni wawili katika klabu ya wanachama binafsi madai yaliyokanushwa awali Johnson kuwa hajawahi kuambiwa juu ya suala lolote dhidi ya Pincher, lakini baadaye alikiri kwamba alikuwa amefahamishwa juu ya suala hilo.

Mawaziri kujiuzulu na wito wa kumtaka kuachia madaraka.
Baada ya Javid na Sunak kujiuzulu, Johnson alikabiliwa na mawaziri kadhaa walioacha kazi zao na kujitenga na uongozi wake na katika hali isiyo ya kawaida baadhi ya mawaziri katika Serikali yake walimtaka ajiuzulu huku wenyewe wakiwa hawajajiuzulu.

Mawaziri hao ni pamoja na mbunge Michael Gove ambaye pia ni mjumbe mkuu wa Brexiteer na mjumbe wa baraza la mawaziri, ambaye alimtaka Johnson ajiuzulu Julai 5, 2022 hali iliyopelekea kufukuzwa kazi, kisha katibu wa mambo ya ndani, Priti Patel inasemekana alimwambia Johnson ajiuzulu lakini yeye akabaki katika wadhifa wake.

Boris Johnson pindi bado hajajiuzulu akiongozana na Katibu Mkuu wake binafsi wa Martin Reynolds baada ya mkutano wa baraza la mawaziri katika Ofisi ya Mambo ya Nje na Jumuiya ya Madola (FCO) huko London, Uingereza Novemba 10, 2020.

Julai 7, 2022 Nadhim Zahawi, aliyetajwa na Johnson kama Kansela mpya siku mbili zilizopita (Julai 6, 2022), naye alimtaka ajiuzulu kwa barua iliyotumwa kwenye mtandao wa Twitter huku Michelle Donelan, aliyeteuliwa kuwa katibu mpya wa elimu Julai 6, 2022, akijiuzulu nafasi yake ya uteuzi ndani ya saa 24.

Nini kitatokea katika serikali ya Uingereza?
Ripoti zilipendekeza kuwa Johnson ataendelea kuwa waziri mkuu hadi msimu wa kiangazi, ili kukipa chama muda wa kumchagua kiongozi mpya inaweza kuamuliwa na chama cha Conservative, ingawa Wahafidhina wengi wameonyesha hasira kwamba Johnson alichagua kung’ang’ania mamlaka kwa muda mrefu badala ya kujiondoa wakati uungwaji mkono wake ulipoanza kuporomoka.

Iwapo Johnson atalazimika kuondoka madarakani bila kujali muda alioutoa wa kumpata mrithi wake, nafasi yake itashikiliwa na Waziri Mkuu wa muda na inakisiwa kuwa kiti chake kitakaliwa na Naibu Waziri Mkuu, Dominic Raab ambaye alitimiza majukumu hayo wakati Johnson alipokuwa Hospitalini kwa maradhi ya Uviko-19, 2020.

Boris Johnson katika viunga vya barabara ya 10 Downing London, nchini Uingereza.

Katika kuchagua kiongozi mpya, Conservatives wanaweza kuanzisha uchaguzi mkuu kutafuta mamlaka kwa mgombea wao, lakini inaarifiwa kuwa wanaweza kumchagua kiongozi mpya wa chama wa ndani, na mtu huyo atakuwa Waziri Mkuu wa Uingereza.

Hata hivyo wapo wagombea wengi wa nafasi ya juu akiwemo Penny Mordaunt, Katibu wa zamani wa ulinzi, Sunak, Zahawi, Javid, na Gove, Katibu wa ulinzi Ben Wallace, Katibu wa mambo ya nje, Liz Truss ambaye shughuli zake na Urusi na Ukraine za hivi karibuni zimempa umaarufu huku Steve Baker mgumu wa Brexiteer, Jeremy Hunt, Katibu wa zamani wa afya, na Suella Braverman ambaye ni mwanasheria mkuu.

Kina Mdee wapeta Mahakama Kuu, waruhusiwa kupinga 'ya CHADEMA'
Tanzania kuandaa AFCON 2027