Naibu Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde ameitaka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), kuhakikisha inafikisha kwa wakati kwa Wakulima matokeo ya tafiti inazozifanya, ili kuongeza tija na kipato chao. 

Mavunde ameyasema hayo hii leo Julai 7, 2022 katika maadhimisho ya siku ya Kilimo Biashara kanda ya Kaskazini yaliyofanyika katika viwanja vya Selian vilivyopo Mkoani Arusha.

“TARI ina jukumu la kufikisha utaalamu na teknolojia wanazozigundua kwa wakulima wetu kwa kutangaza matokeo na teknolojia hizo ili ziweze kuwa na tija kubwa kwa wakulima,” amesisitiza Naibu Waziri.

Amesema, watafiti ni lazima waache utaratibu wa kufungia au kukaa  na matokeo ya tafiti na teknolojia maofisini, badala yake wanatakiwa kujikita katika ubunifu wa kufikisha utaalamu huo kwa wakulima. 

Mavunde ameongeza kuwa, “Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetupa kipaumbele cha kipekee sisi wakulima, na ndo maana bajeti ya Wizara ya Kilimo imeongezeka kutoka bilioni 294 mwaka 2021/2022 hadi bilioni 954 mwaka 2022/2023.”

Hata hivyo, amebainisha kuwa bajeti iliyoongezeka imeelekezwa katika utekelezaji wa vipaumbele vya kimkakati, ikiwemo kuimarisha utafiti, kuongeza uzalishaji wa mbegu bora ili kuongeza mavuno kwa wakulima sambamba na ugunduzi wa mbinu bora za kilimo zitakazo msaidia mkulima wa Tanzania kuzalisha kwa tija.

Akiongea katika eneo hilo, Mkurugenzi Mkuu wa TARI, Dkt. Geoffrey  amesma wamepokea maelekezo ya Naibu Waziri Mavunde na kwamba tayari wameanza utekelezaji wake.

Ameutaja utekelezajinhuo kuwa ni pamoja na kuanzisha maadhimisho ya siku ya kilimo biashara katika vituo vyote vya Kanda vya Utafiti na Viwanja vya Nanenane Nchi nzima, ili kufikisha matokeo ya tafiti mbalimbali kwa wakulima kwa lingo la kusaidia Kilimo chenye tija.

Habari kuu kwenye magazeti ya leo Julai 8, 2022
Wachimba madini watakiwa kusafisha Dhahabu nchini