Klabu ya Ajax ina matumaini makubwa ya kuipata saini ya kiungo wa Al Etifaq, Jordan Henderson kwa mkopo wa nusu msimu licha ya kuwepo kwa upinzani kutoka Juventus na Etifaq yenyewe ambayo imesisitiza haina mpango wa kumuuza.

Mabosi wa Ajax wanapambana kutaka kuboresha kikosi chao katika dirisha hili baada ya kuanza vibaya ambapo kwa sasa wanashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi.

Henderson mwenye umri wa miaka 33, mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2026, amekuwa akihitaji kuondoka nchini Saudi Arabia ikiwa ni miezi kadhaa tu tangu atue nchini humo na kinachoelezwa ni hana furaha.

Mabosi wa Etifaq hivi karibuni wameripotiwa kuwa hawana mpango kumtoa kwa mkopo staa huyu anayekunja Pauni 700,000 kwa wiki licha ya tetesi zinazosambaa.

Baadhi ya ripoti zinadai Henderson huenda akarejea nchini England ambako pia kuna timu nyingi zinazohitaji kumsajili kwa mkopo.

Mazingira bora uwekezaji yaivutia AngloGold Ashanti kuwekeza Nchini
Wawili wamfuata Francis Baraza Dodoma Jiji