Kocha Mkuu wa AS Roma Jose Mourinho amesema haelewi ni kwa nini alioneshwa kadi nyekundu kwa kutoa ishara ya kulia kuelekea mwisho wa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Monza mwishoni mwa juma lililopita (Jumapili – Oktoba 22).
Bao la dakika ya 90 kutoka kwa Stephan El Shaarawy liliwahakikishia AS Roma ushindi dhidi ya Monza, ambao walikuwa na wachezaji 10 baada ya Danilo D’Ambrosio kutolewa kipindi cha kwanza.
Mourinho alioneshwa kadi nyekundu dakika za lala salama baada ya kuonekana akionesha ishara ya kulia kuelekea makocha wa Monza.
“Sijui kwa nini nilipata kadi nyekundu, nilionesha ishara tu kwa benchi, hakuna hata neno moja,” amesema Mourinho.
“Benchi la Monza liliweka shinikizo kubwa kwa mwamuzi, hawakupaswa kuwa na tabia kama hiyo.”
Akiwa na kadi nyekundu, Mourinho hatakuwa kwenye benchi katika mechi inayofuata ya ligi ya AS Roma ugenini dhidi ya klabu yake ya zamani Inter Milan.
Licha ya kuonekana kuwakejeli wakufunzi wa Monza, Mourinho alitoa sifa tele kwa timu ngeni.
“Hawakustahili kupoteza mchezo,” alisema Mourinho.
“Timu yangu ilikuwa kwenye matatizo kila mara, tulifanya makosa mengi na tuliteseka. Ulikuwa ni mchezo wenye kiwango cha chini cha kiufundi lakini chenye hisia za juu.