Maafisa wa uchaguzi nchini Nigeria wamefanya uidhinishaji wa kibayometriki kwa wapiga kura kabla ya uchaguzi wa rais na bunge kuanza Februari 25, 2023.
Nigeria inatarajia kumchagua mrithi wa Rais Muhammadu Buhari ambapo magavana wa majimbo na wabunge watachaguliwa wiki mbili baadaye huku Tume Huru ya Kitaifa ya Uchaguzi (INEC), ikianzisha mfumo wa kuidhinisha wapiga kura katika kura za 2015 na 2019.
Kamishna wa Uchaguzi wa Jimbo la Lagos, Olusegun Agbaje amesema “hii ni kuijaribu BVAS kazi ya BVAS ni kutoa vibali vya watu usoni au kwa uchapaji wa vidole gumba, ikiwa huwezi kufanya alama ya kidole, basi tunatoa usoni ili kutuwezesha kujua kuwa wewe ndiye mmiliki halisi wa kadi iliyotolewa na INEC”.
Baadhi ya wapiga kura walifurahia zoezi hilo na alama zao za kibayometriki kuchukuliwa na maafisa wa INEC ili kusaidia kuboresha maandalizi ya uchaguzi mkuu.