Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amesema kuwa hakuna mwenye uhakika wa cheo katika serikali ya awamu ya tano kwani hata yeye mwenyewe hana uhakika kama atakuwa Rais wa muda wote na kuwataka viongozi kushughulika na matatizo ya wananchi mapema na sio kumsubiri yeye kuyatatua.
Ameyasema hayo jana Agosti Mosi, 2018 Ikulu jijini Dar es salaam wakati akihutubia mara baada ya kuwaapisha wakuu wa mikoa, makatibu tawala, makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu.
“Hizi kazi sisi sote tumepewa dhamana. Mimi mwenyewe pia nimepewa dhamana, hakuna mwenye uhakika na kazi hizi hata mimi sina uhakika na kazi hizi kwamba nitakuwa Rais wa moja kwa moja. Hii ni kazi ngumu, Hii ni kazi ni ngumu, its terrible job. Leo tu mimi nimeamka saa nane usiku usiku mara IGP ananipigia simu anasema kuna watu wetu wamepata ajali mpakani, kuna mwingine anasema hivi,”amesema Rais Dkt. Magufuli
Aidha, Rais Magufuli ameonyesha kuchukuziwa na kitendo cha jiji la Dar es Salaam kushika nafasi ya mwisho katika ukusanyaji wa mapato katika majiji sita.
Hata hivyo, Rais Dkt. Magufuli ameongeza kuwa jinsi hali inavyoendelea wataweka mikakati ya kushusha hadhi ya majiji ambayo yatakuwa yanashindwa kufikisha malengo yake ya kimapato yaliyowekwa.
-
Video: Waziri Mhagama atangaza rasmi kuanza utekelezaji wa sheria mpya PSSSF
-
Video: Polisi wafunguka kuhusu kumkamata Zitto Kabwe, “Tunafanya kazi kwa weledi
-
Video: Polisi wakanusha madai ya mbwa kupotea, ‘alikuwa masomoni’