Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli amemuagiza Waziri wa Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi William Vangimembe Lukuvi kufuta umiliki wamashamba mawili makubwa katika eneo la kigamboni na kuyarudisha serikalini likiwemo la Amadol lenye ekari 5,400 na lililokuwa likimilikiwa na mfanyabiashara Yusuf Manji lenye ekari 715.
Pia amesitisha na kuvunja mamlaka ya uendelezaji wa mji wa kigamboni (KDA) kuanzia leo septemba 13.
‘Rais ameniagiza niwaalifu kuwa leo amevunja rasmi KDA ’amesema Lukuvi.
Hayo yamezungumzwa leo katika ukumbi wa chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.
-
Kaskazini Pemba yaanza kutekeleza maagizo ya Rais Dkt. Shein
-
Kilimo cha kupindukia husababisha Jangwa
Mkuu wa Wilaya Kigamboni, Hashim Mgandilwa amethibitisha hilo na kusema kuwa Rais JPM ni msikivu kwani amesikia kilio cha watu wa kigamboni na kuamua kuvunja mamlaka hiyo ya uendelezaji wa Mji wa Kigamboni (KDA).
Amesema ‘Usikuvu ni sehemu ya utatuzi hatimaye Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli aridhia uvunjwaji wa Mamlaka ya uendeshaji Mji wa Kigamboni” Mgandilwa.
Ambapo mwaka jana Mbunge wa Kigamboni, Faustine Ndugulile aliomba shughuli zote za undelezaji mji wa Kigamboni zikabidhiwe kwa Halmashauri ya Manispaa hiyo ili kuendeleza mji