Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kumwakilisha katika sherehe za uapisho wa Rais Mteule wa Jamhuri ya Zimbabwe, Emmarson Dambudzo Mnangagwa zitakazofanyika tarehe 26 Agosti 2018 jijini Harare.

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete ataongozana na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Bara, Philipo Mangula na Mwenyekiti wa Chama Cha UDP, John Momosa Cheyo.

Aidha, Rais Mnangagwa ataapishwa kesho kuingoza Zimbabwe baada ya kushinda katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 30 Julai 2018 akiwa anapokea kijiti kutoka kwa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Robert Mugabe.

 

 

Mimi sipiganii CCM wala Chadema, niacheni- Musiba
Nzega yamchefua Makamba, atoa maagizo makali