Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa anapatwa na kigugumizi kusaini hukumu za wafungwa ambao wamehukumiwa kunyongwa baada ya kukutwa na makosa mbalimbali.
Ameyasema hayo hii leo Ikulu Jijijni Dar es salaam wakati wa hafla ya kumwapisha Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Hamis Juma, ambapo amemtaka Jaji huyo kusimamia haki katika kutoa maamuzi.
Amesema kuwa anatambua kuwa idadi wa wafungwa waliohukumiwa kunyongwa ni wengi sana ila anaomba asipewe hiyo orodha kwakuwa kutoa maamuzi ya kusaini hukumu hiyo itakuwa ni ngumu.
“Sisi wanasiasa tunaogopa kunyonga, natambua kuwa sasa orodha ya watu ambao wanatakiwa kunyongwa ni kubwa sana ila mimi naomba hiyo orodha msiniletee kwa sababu najua ugumu wake ulivyo,”amesema Rais Dkt. Magufuli
-
Maswali 10 yanayomkabili dereva wa Lissu
-
Video: JPM amuapisha Prof. Ibrahim kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania
- Familia yasusa mazishi ya mteka watoto Arusha
Hata hivyo, Rais Magufuli amesema kuwa amechukua muda mrefu kumteua Jaji Mkuu wa Tanzania kutokana na ukweli kwamba alikuwa anatafuta mtu ambaye anaweza kuendana na dhamira yake ya kupambana na rushwa hivyo alipojilidhisha na jaji huyo ndiyo akaamua kumteua kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania.