Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Prof. Ibrahim Hamis Juma kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania, mara baada ya kukaimu nafasi hiyo kwa muda mrefu.

Profesa Ibrahim Hamis Juma alikuwa kabla ya kuteuliwa na kuapishwa alikuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania ambapo alichukua nafasi hiyo kutoka kwa Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman ambaye amestaafu.

Aidha, mara baada ya kumuapisha Jaji Mkuu wa Tanzania, Rais Magufuli amemtaka Prof. Juma kufanya kazi kwa kusimamia maadili pia kusimamia haki kwa kupambana na rushwa.

“Nimekuteua Jaji Prof. Juma kwa kuangalia mambo mengi, hivyo kawatumikie wananchi kwa kusimamia haki katika utekelezaji wa majukumu yako ya maamuzi ambayo yataleta tija katika Taifa,”amesema Rais Dkt. Magufuli

Hata hivyo, Rais Magufuli amevitaka vyombo mbalimbali vinavyosimamia sheria kukaa kwa pamoja ili kuweza kujadili changamoto ambazo zimekuwa zikiwakabili ili kuweza kuharakisha kutolewa kwa maamuzi.

 

Familia yasusa mazishi ya mteka watoto Arusha
Maswali 10 yanayomkabili dereva wa Lissu