Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kufuatia vifo vya Wanafunzi 29 na walimu 4 wa shule ya msingi ya Lucky Vicent Arusha.

Rais Magufuli ameeleza kusikitishwa na ajali hiyo kwani imezima ndoto za watoto waliokuwa wakijiandaa kulitumikia Taifa na imesababisha uchungu, huzuni na masikitiko makubwa kwa familia za marehemu na Taifa kwa ujumla.

“Ndg Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo naomba unifikishie pole nyingi kwa wazazi, ndugu, jamaa na marafiki wote wa wanafunzi, walimu na dereva waliopoteza maisha, hiki ni kipindi kigumu kwetu sote, na uwaambie naungana nao katika majonzi na maombi.

Rais Magufuli amesema kuwa kitu cha muhimu kwa sasa tuwaombee marehemu wote wapumzishwe mahali pema, majeruhi wapone haraka na wote walioguswa na msiba huu wawe na moyo wa subira.

“Muhimu kwa sasa tuwaombee marehemu wote wapumzishwe mahali pema, majeruhi wapone haraka na wote walioguswa na msiba huu wawe na moyo wa subira, ustahimilivu na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu” Amesema Rais Magufuli.

Mwakyembe atoa ushauri huu kwa wanamichezo
Waziri Mwigulu, Zitto watoa pole vifo vya wanafunzi, walimu Arusha