Wanamichezo nchini wameshauriwa kupata chanjo ya homa ya manjano kabla ya kusafiri ili kujikinga dhidi ya ugonjwa wa homa ya manjano wanapokwenda nchi ambazo zina maambukizi ya ugonjwa.

Ushauri huo umetolewa na Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe mara baada ya kupata chanjo hiyo katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.

Amesema kuwa wanamichezo wanastahili kupata chanjo hiyo ili wasipate ugonjwa pindi wanapotembelea nchi zenye ugonjwa huo.

“Nawaomba wanamichezo na watanzania kwa ujumla wapate chanjo hii ili kusudi wajilinde kutokupata ugonjwa huu kwani tumezungukwa na nchi wanachama ambao wana  ugonjwa wa homa ya manjano” amesema Dkt. Mwakyembe.

Hata hivyo, kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbas Amesema kuwa  ugonjwa wa homa ya manjano una madhara  hivyo ni vyema kwa wafanyakazi,wafanyabiashara pamoja na  wanafunzi wanaosafiri nje ya nchi hususani nchi zenye ugonjwa huo ni vyema wakajitokeza kupata chanjo

Video: DC Mjema azungumza na wenyeviti kuhusu ulipaji kodi za majengo
JPM atuma salamu za rambirambi Arusha, ni kufuatia vifo vya wanafunzi, walimu