Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amesema kuwa zoezi la ulipaji kodi za majengo katika wilaya hiyo ni la lazima na litaendeshwa kwa utaratibu maalum kulingana na maeneo husika.

Ameyasema hayo mapema hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na wenyeviti wa Serikali za mitaa kutoka kata mbalimbali za wilaya ya Ilala.

“Tumewaita hapa wenyeviti ili kuweza kuwapa semina na kuondoa mkanganyiko ambao umekuwa ukijitokeza kwa wananchi kuhusu utaratibu wa ulipaji kodi za majengo, naamini wametuelewa kwa sasa kilichobaki ni wao kwenda kutoa semina kwa wananchi,”amesema Mjema.

Hata hivyo, Mjema ametoa tahadhari kwa mtu yeyote atakaye jaribu kukwamisha zoezi hilo kwani ulipaji wa kodi ni mhimu kwa kuwa ndiyo inayodharisha mahitaji yote ya muhimu.

Magazeti ya Tanzania leo Mei 7, 2017
Mwakyembe atoa ushauri huu kwa wanamichezo